Tuesday, March 8, 2011

Barcelona nyumbani na Ze Gannazzzz leo....

Hawa wamo katika mchezo wa leo, Nahodha Cesc Fabregas na Mshambuliaji Robin Van Persie.

Arsenal leo wanakutana na Barcelona Camp Nou katika mchezo wa marudiano, baada ya Arsenal kutoka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Emirates.
Arsenal leo ikiwa kama itafanikiwa kutoka sare ya kutofungana, itakuwa imesonga mbele katika mashindano haya ya klabu bingwa barani Ulaya na itabakia Swa kuwa maana pekee kwa sare nyingine yoyote ya magoli ambayo Arsene Wenger na vijana wake watakayoilazimisha kule Hispania.

Swali ni kuwa je wataweza..... inawezekana kama ilivyowezekana kwao na hata ushindi pia unawezekana, ndiyo imani ya Wenger na vijana wake.

Kocha wa Barcelona Pep Guardiola kwa upande wake amekisifia sana kikosi hichi cha Arsenal anasema ni wakali na wamedumu kuwa timu bora kwani kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakishiriki klabu bingwa ulaya na kubaki kuwa moja ya timu tatu bora za Uingereza kwa hili anasema hawatawabeza....

Pamoja na uhakika wa nahodha Cesc kucheza uwanja wake wa zamani nyumbani na Van Persie, Bakari Sangna atakuwa na wakati mgumu wa kukabiliana na Leonel Messi ambaye kiungo mwezie Muargentina Marcherano anasema leo atagonga goli tano.

Michezo mwingine utakaochezwa leo ni:

Shakhtar Donetsk vs As Roma

Monday, March 7, 2011

Huyu aligoma kabisa kuzungumza na Vyombo vya Habari......

Sir Alex Ferguson amegoma....

Mpasuko wa Nani.......eehh wamemnaniii

Hapa jeraha la Nani likionekana kwa karibu zaidi......

Kuyt agonga "Hat Trick"

Mdachi baada ya kungonga tatu Mdachi mwezie.....au jezi ya Kipa wa Manchester United ilileta gundu?
a

Nani Kaumia Kweli.......

Sehemu ya Mguu wa Loius Nani ikionyesha alivyochanika nyama ya ugoko baada ya kukwatuliwa na beki mkongwe wa Liverpool Jimmy Carragher, jeraha ambalo lilisababisha winga huyu mshabuliaji kuharakishwa nje ya uwanja kwa matibabu....Imefahamika kuwa Beki huyo alikwenda kumuomba radhi katika chumba cha kubadilishia nguo wachezaji.

Sunday, March 6, 2011

MICHAPO IMERUDI

Asalaam aleikum ndugu zangu wote......

Baada ya kimya cha muda mrefu naomba niwashukuru kwa kuwa pamoja nami katika Jahazi...

Mwaka jana tunamshukuru Mwenyezi Mungu alituwezesha kuuvuka salama salmini na sasa tukiwa mwezi huu wa tatu mwaka 2011, ni mwaka kamili toka tupeane michapo katika Blog yetu hii.

Naahidi kwa Rehema zake YEHOVA Mungu wetu, tutaendelea kupeana michapo hapa katika Blog yetu. Huku tukipanua wigo zaidi ya sekta ya michezo pekee, na kwenda kuzunguka kugusa maswala yenye mvuto katika jamii ya Kitanzania.

Michango yenu ya mawazo na mawsali yatakaribishwa sana katika kurasa yetu ya michapo, na kuwekwa hadharani kwa faida ya mafunzo na uwelewa zaidi wa Mtazania.

Pamoja na Blog hii, kuweka hadharani maoni yenu na maswali, pia natarajia kuyajumuisha katika Jahazi letu la jioni kila siku za kazi za wiki na pia Katika "KIBONDE SHOW" seasson two inayokuja hivi karibuni ambayo kama kawaida itakuwa ikiruka hewani mara moja kwa wiki kupitia CLOUDS TV.

Asalaam aleikum na Karibuni nasa tuwe sote.

Ephraim Samson Kibonde.




Tuesday, March 2, 2010

Deco: Carlo Ancelotti niache niondoke!


Kiungo wa kimataifa raia wa Ureno DECO, amemtaka Carlo Ancelotti kumruhusu aondoke zake pale darajani, almaarufu kama klabu ya Chelsea.
Hili litakuwa ni pigo jingine kwa "The Blues" baada ya kipigo cha Inter Milan, pamoja na kashfa za nahodha, John Terry na Ashley.

Na hiki ndicho Deco anachosema : "Nataka kurejea Brazil" kwani bado ninahisi kuwa nina uwezo wa kucheza katika kiwango cha juu katika kandanda na la ziada ni kuwa ninatamani kuwa karibu na watoto wangu.
Deco,ambaye sasa ana umri wa miaka thelathini na mbili (32),bado mkataba wake unadai utumishi wake kwa Chelsea kwa mwaka mwingine mmoja.
Hata hivyo anaweka wazi uamuzi wake huo, kuwa angependa utimie baada ya fainali za kombe la dunia.

akiwa ni baba wa watoto wanne, Deco amekuwa ni kiungo muhimu sana katika klabu ya Chelsea chini ya boss Ancelotti, akicheza michezo ishirini na nne (24) msimu huu.
Akionyesha kuwa amekomaa kama mchezaji wa kulipwa, Deco anasema kuondoka kwake kutategemea sana uamuzi wa klabu yake ya Chelsea., ikiwa kama watamuachia aondoke hata kama kwa mkopo.
Flamengo ni moja ya timu ambayo imeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyu wa kireno , Mzaliwa wa Brazil ambaye amepanga kustaafu soka la kimataifa baada ya kombe la dunia.

Promoter FRANK WARREN amzungumzia MIKE TYSON


MIKE TYSON sasa yuko mbioni kuorodheshwa, kisha kutamkwa kuwa mmoja kati wale walio katika orodha ya mabondia wakuheshimiwa na kukumbukwa duniani.
Huku hili linatarajiwa kutamkwa rasmi baadae mwaka huu tayari baadhi ya wadau wa mchezo wa masumbwi duniani wameanza kulizungumzia, huku wakihoji juu ya uamuzi huo.

Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa katika maswala ya masumbwi Tyson ataendelea kustahili milele, kwani bado anashikilia rekodi ya kuwa Bingwa wa Dunia wa masumbwi ya uzito wa juu akiwa na umri mdogo na huo aliupata katika miaka ya 1980.

Pamoja na ubingwa huo, Iron Mike pia amekuwa ni bondia maarufu sana katika historia ya wanamichezo duniani.

Wadau je mnakumbuka enzi za kusubiri masumbwi hadi saa kumi na moja za alfajiri pale Palm Beach hotel....palikuwa panaitwaje tena.....? 'SUGAR RAYS"

Itakumbukwa kuwa baada ya kutumikia kifungo, kutokana na kosa la kubaka, Tyson alirejea ulingoni akiwa na nia moja tu ya kurejesha tena mikanda yake ya ubingwa wa dunia uzito wa juu.

Kipindi hicho kilipita huku mashabiki wa ngumi bila ya kujali atashinda au atashindwa walisubiri kwa hamu mapambano yake.
Nakiri kuwa wachache kati yetu watajisahaulisha yale mapambano mawili ya Tyson dhidi ya Evander Holyfield, kwa nia njema na mbaya.

Inagawa lile pambano alilochapwa na James 'Buster' Douglas miaka ishirini iliyopita kwa hakika, liliusitua ulimwengu na si la kusahaulika.

Kiutamaduni Mike Tyson,ambaye sasa ana umri wa maiaka arobaini a tatu (43),atabaki akikumbukwa sana duniani kwa mengi mazuri na mabaya kuliko mwanamichezo mwingine yeyote katika kizazi tunachoishi.

Sasa basi, kuhoji kwa wadau kunakuja baada ya kuangalia kile ambacho bondia huyu amekuwa akikifanya nje ya ulingo, mmoja wao akiwa ni Promota anayeheshimika sana nchini Uingereza na duniani Frank Warren.

Anasema ameshawahi kukutana na Tyson mara kadhaa na anachoweza kusema ni kuwa bondia huyu, mara nyingine huwa ni mchangamfu sana na utamfurahia lakini wakati mwingine unaweza kuogofywa naye.

Promota huyu anasema yale mabaya yasihesabiwe kwa Tyson na atangazwe kuwa mmoja wa mabondia bora waliowahi kuishi duniani na akahoji kwani Sonny Liston alikuwa malaika?

Wengi wengine waliohoji juu ya Tyson inaonekana wazi kuwa wanamhusisha na kashfa za ngono amabazo zimekuwa zikiwaandama wanamichezo kama John Terry, Ashley Cole na Tiger Woods.

Lakini vyovyote vile jamani katika ulimwengu huu, ni nani ambaye anaweza akasimama na kunyooshea kidole mwenzie kuwa ni mbaya wakati ana ya kwakwe ambayo hayajawekwa wazi tu.

Tyson hakuamka asubuhi na kuwa bondia mkali katika masumbwi, alifanya kazi ya ziada, alijituma akapambana na kufikia kuwa Bondia mdogo kuliko wote kutwaa ubingwa wa dunia uzito wa juu.

Monday, March 1, 2010

Pole Sana Aaron Ramsey!

Pole sana Aaron Ramsey, unaweza sema ni mpira tu lakini ni kwa nini itokeee kwa wachezaji wa Arsenal tu? je ni umri au lishe duni?

Monday, February 22, 2010

Thursday, February 18, 2010